KUSHIRIKIANA NA IDARA YA BILI: Ninaelewa kwamba ingawa Vituo vya Afya vya Five Rivers huenda vikanisaidia kufanya haya, ninawajibika mwenyewe kufuata masharti ya hati ya bima yangu, ikiwemo kuthibitisha bima na kupata cheti/hati yoyote inayohitajika ya kabla ya kulazwa. Ninakubali kushirikiana kikamilifu na Vituo vya Afya vya Five Rivers katika kutuma bili kwa kampuni yangu ya bima na mlipaji mwingine yeyote asiyehusika moja kwa moja, ikiwemo, bali sio tu, kujibu haraka maombi ya taarifa kutoka kwa Vituo vya Afya vya Five Rivers, ama mweka kampuni ya bima yeyote ama mlipaji mwingine asiyehusika moja kwa moja haraka. Ninaelewa pia kwamba ili nipokee usaidizi wowote wa kifedha wa kulipa bili yangu, lazima nikamilishe maombi yote yanayohitajika, nitoe hati za kuthibitisha taarifa zilizoombwa na nitimize mahitaji mengine yote ya mpango wa usaidizi haraka kwa kwa ukweli. Ninakubali kwamba nikikataa kushiriki katika masuala haya huenda ninymwe manufaa ama usaidizi/msaada. Mweka kampuni ya bima yeyote ama mlipaji
mwingine asiyehusika moja kwa moja akikataa kulipa dai la Vituo vya Afya vya Five Rivers; Nitatimiza haraka michakato yote ya kufuatilia malipo hayo
ambayo ninaweza kutimiza. Pia ninapeana ruhusa ili Vituo vya Afya vya Five Rivers vifuatilie malipo ya dai hilo kwa niaba yangu. Ninakubali, ili Vituo vya
Afya vya Five Rivers viweke pesa kwenye akaunti yangu ama vikusanye viwango vyovyote ambavyo huenda ninadaiwa, Vituo vya Afya vya Five Rivers
vinaweza kuwasiliana na mimi kupitia simu kwa namba yoyote ya simu inayohusiana na akaunti yangu, ikiwemo namba za simu za mkononi, na pia vinaweza kuwasiliana na mimi kwa kutuma ujumbe mfupi au barua pepe, kupitia anwani yoyote ya barua pepe ninayotoa itumike ambayo inaweza kusababisha nitozwe ada fulani. Mbinu za kuwasiliana zinaweza kujumuisha kutumia ujumbe wa sauti uliorekodiwa kitambo/bandia na/ama kutumia kifaa cha kupiga simu kiotomatiki, inavyofaa.