Kuchelewa Kufuta Miadi
Ni lazima upige simu ndio ufute miadi iliyoratibiwa kabla ya miadi hiyo ndio isichukuliwe kwamba “hukufika”
Kutofika
Unaweza kufukuzwa kutoka kwa maeneo yote ya FRHC ikiwa hujafika kwa miadi mitatu (3) iliyoratibiwa. Wagonjwa waliofukuzwa wanaweza kukubaliwa tena kama wagonjwa kama tu wameshaonwa kwa ziara 3 za kujileta/kufanya ndani.
Sera za Bima/kifedha
Malipo funge inafaa kulipwa wakati wa huduma.
Kuchelewa kwa miadi
Ikiwa utachelewa kwa zaidi ya dakika 15 kwa miadi yako, huenda hautaonwa na itabidi upange miadi ingine.
Fomu
Wahudumu wa FRHC watajaza fomu za wagonjwa ndani ya siku 7-10 baada ya kuzipokea kulingana na fursa watakaopata
Tabia/ Maadili
Kutumia lugha chafu, kutusi kwa maneno au tabia zinazotisha kwa wafanyakazi, wahudumu na au wagonjwa zinaweza kuwa sababu za kukufukuza kutoka maeneo yote ya FRHC.
Rekodi
Kutakuwa na ada za nakala za rekodi za kimatibabu ulizopatiwa Hakuna malipo yatakayotozwa ikiwa nakala za rekodi zitaombwa na kutumwa moja kwa moja kwa muhudumu mwingine.
Picha/ Video/ Kurekodi Sauti
Kupiga picha/ kurekodi video au kurekodi sauti (bila idhini) kumepigwa marufuku kwa mgonjwa yeyote, mwanafamilia au mgeni katika eneo lolote la Vituo vya Afya ya Five Rivers.
Bunduki/ Silaha
Bunduki na silaha nyingine hazikubaliki katika mali ya FRHC.
Kutobagua Wafanyakazi kwa msingi wa Umri, Jinsia, Rangi, Dini, Hisia za Kimapenzi kwa Usalama wa Wagonjwa
FRHC itafanya kila juhudi ili kushughulikia mahitaji ya kitamaduni na kidini ya mgonjwa na maombi bora tu usalama na hali ya huduma ya mgonjwa isiathirike.
Tunawaomba wagonjwa wetu wazingatie yafuatayo ndio iwe wamefuata Kanuni ya Maadili.
Hakuna kutumia lugha chafu katika ofisi. Tafadhali usizungumze kupitia simu, ukiwa katika maeneo ya usajili na huduma kwa wagonjwa. Tafadhali wajulishe jamaa na marafiki ili wao pia watii kanuni ya maadili.